Friday, February 1, 2013


Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil Paint. 

Hii Picha ilinirudisha mawazo yangu nyuma kabisa mnamo miaka ya 84 mpaka 90 wakati nilipokua naishi Wilaya ya Pangani.
Katika wilaya hiyo kuna sehemu inaitwa Mauya, ni maharufu sana kwa kilimo cha minazi, nami ndio ilikua kimbilo langu pindi tu ifikapo siku za Ijumaa nilikwenda kutumika kazi  ndogo ndogo za kukusanya nazi zilizo anguliwa na Wakwezi.
Mbali na kazi hizo, pia nilipenda sana kuvua samaki wa kitoweo kwani walipatikana kwa urahisi zaidi. Shughuli mbali mbali zilifanyika na usafiri wao mkubwa ni wa njia ya mto Pangani.   Ni eneo ambalo kama lingeandaliwa vizuri nafikiri hata shughuli za kitalii lingewezekana kufanyika.
Twendeni sasa tukaone maajabu nilioyaona mimi.
       Twende sasa na Artist Hendry Lilanga

Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil Paint.

Akili moja, mawazo yanayo fanana, ila utendaji kwetu bado ni mgumu sana katika makazi yetu!  Kila tuliempelekea haya mawazo yetu  waliyakubali,  ila mioyoni mwao waliogopa!

Sababu ya kuogopa kwao,  Walizoea siku zote tuwe nyuma yao hata kama hawana huwezo huo.  Mimi na Manju tumebaki na Vipaji vyetu, na wao wamebaki na Pesa zao.    Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.
Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil paint.