Friday, April 19, 2013

Nionavyo Mimi!
   
              Sanaa za kazi za mikono katika Nchi yangu inaonekana ni kama mchezo wa makida makida! Sometime unashindwa hata kujitambulisha kwenye alaiki ya watu kua wewe ni aidha Mchoraji au Mchongaji pengine Mcheza  ngoma za utamaduni.    

               Msanii katika Nchi yangu amekua ni kiburudisho tu, pale panapotokea wageni toka labda nje ya nchi, ama katika makongamano tofauti tofauti  hapa Msanii huwa na thamani kiasi fulani,  lakini baada ya kumaliza matakwa yao!  Msanii huendelea kuonekana kama kituko cha mtaa au janvi la wageni tu.

                Hali ni mbaya sana kwa wasanii ya Uchongaji na hata Wachoraji,  nionavyo Mimi ikiwa Ukoo wako hawakutaki basi hata huendako ni kazi bure. Nchi iliyokua na kila kitu lakini imekua ndio inayoonekana haina kitu!  Nafikri kwa hali hii sasa, ni lazima tuzungumze.

                 Artist Hendry Lilanga katika Nchi yangu.
FAMILIA IKIKOSA MSIMAMO WA KUPANGA MAISHA YA MPANGILIO, SHIDA KUBWA HUJA KUMUELEMEA MAMA,   SABABU YEYE NDIE HASA MWENYE UCHUNGU WA FAMILIA YAKE WAKATI WOTE.     BABA FAMILIA SIKUZOTE HUTAFUTA NJIA YA KUKWEPA MAJUKUMU NA NDIPO VINAPOANZA VISINGIZIO KIBAO ILIMRADI TU KUMUACHIA MAMA FAMILIA MZIGO WA KULEA WATOTO WAKE.    TABIA HII SIO NZURI HATA KIDOGO,  NAOMBA AKINA BABA TUWASAIDIE MAMA ZETU MAJUKUMU YA KULEA FAMILIA ZETU.
KAKA AMEAMUA KUWASUBIRI WADOGOZAKE WALIOAMUA KUPUMZIKA.

WAMETOKA MBALI NA WANAKWENDA MBALI KUMTEMBELEA BIBI YAO SABABU HAWAJAMUONA SIKU NYINGI.   NA HAPO KAKA ANAFIKILIA JINSI ALIVYOWACHOSHA WADOGOZAAKE,  ANAWAONEA HURUMA.

Friday, February 1, 2013


Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil Paint. 

Hii Picha ilinirudisha mawazo yangu nyuma kabisa mnamo miaka ya 84 mpaka 90 wakati nilipokua naishi Wilaya ya Pangani.
Katika wilaya hiyo kuna sehemu inaitwa Mauya, ni maharufu sana kwa kilimo cha minazi, nami ndio ilikua kimbilo langu pindi tu ifikapo siku za Ijumaa nilikwenda kutumika kazi  ndogo ndogo za kukusanya nazi zilizo anguliwa na Wakwezi.
Mbali na kazi hizo, pia nilipenda sana kuvua samaki wa kitoweo kwani walipatikana kwa urahisi zaidi. Shughuli mbali mbali zilifanyika na usafiri wao mkubwa ni wa njia ya mto Pangani.   Ni eneo ambalo kama lingeandaliwa vizuri nafikiri hata shughuli za kitalii lingewezekana kufanyika.
Twendeni sasa tukaone maajabu nilioyaona mimi.
       Twende sasa na Artist Hendry Lilanga

Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil Paint.

Akili moja, mawazo yanayo fanana, ila utendaji kwetu bado ni mgumu sana katika makazi yetu!  Kila tuliempelekea haya mawazo yetu  waliyakubali,  ila mioyoni mwao waliogopa!

Sababu ya kuogopa kwao,  Walizoea siku zote tuwe nyuma yao hata kama hawana huwezo huo.  Mimi na Manju tumebaki na Vipaji vyetu, na wao wamebaki na Pesa zao.    Ama kweli usilolijua ni sawa na usiku wa kiza.
Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil paint.