Friday, April 19, 2013

Nionavyo Mimi!
   
              Sanaa za kazi za mikono katika Nchi yangu inaonekana ni kama mchezo wa makida makida! Sometime unashindwa hata kujitambulisha kwenye alaiki ya watu kua wewe ni aidha Mchoraji au Mchongaji pengine Mcheza  ngoma za utamaduni.    

               Msanii katika Nchi yangu amekua ni kiburudisho tu, pale panapotokea wageni toka labda nje ya nchi, ama katika makongamano tofauti tofauti  hapa Msanii huwa na thamani kiasi fulani,  lakini baada ya kumaliza matakwa yao!  Msanii huendelea kuonekana kama kituko cha mtaa au janvi la wageni tu.

                Hali ni mbaya sana kwa wasanii ya Uchongaji na hata Wachoraji,  nionavyo Mimi ikiwa Ukoo wako hawakutaki basi hata huendako ni kazi bure. Nchi iliyokua na kila kitu lakini imekua ndio inayoonekana haina kitu!  Nafikri kwa hali hii sasa, ni lazima tuzungumze.

                 Artist Hendry Lilanga katika Nchi yangu.

No comments:

Post a Comment