Hendry Lilanga Paint
The size 100cm by 100cm Oil Paint.
Hii Picha ilinirudisha mawazo yangu nyuma kabisa mnamo miaka ya 84 mpaka 90 wakati nilipokua naishi Wilaya ya Pangani.
Katika wilaya hiyo kuna sehemu inaitwa Mauya, ni maharufu sana kwa kilimo cha minazi, nami ndio ilikua kimbilo langu pindi tu ifikapo siku za Ijumaa nilikwenda kutumika kazi ndogo ndogo za kukusanya nazi zilizo anguliwa na Wakwezi.
Mbali na kazi hizo, pia nilipenda sana kuvua samaki wa kitoweo kwani walipatikana kwa urahisi zaidi. Shughuli mbali mbali zilifanyika na usafiri wao mkubwa ni wa njia ya mto Pangani. Ni eneo ambalo kama lingeandaliwa vizuri nafikiri hata shughuli za kitalii lingewezekana kufanyika.
Twendeni sasa tukaone maajabu nilioyaona mimi.
Twende sasa na Artist Hendry Lilanga
No comments:
Post a Comment