Tuesday, November 30, 2010
Baadhi ya Vyombo vya habari Tanzania ndio maadui wakubwa wanao waangamiza Wasanii kisanaa. Tarehe 29/11/2010 kuna radio moja wapo maharufu sana hapa Tanzania hurusha kipindi cha Jahazi niliwasikia wakishabikia uhuzwaji wa Nyumba ya Sanaa yakua ni sahihi kwani hata wao pia eti hawaoni sanaa yoyote hapo nyumba ya sanaa! na nibora ivunjwe na pajengwe Ghorofa kwani sasa sanaa hakuna chochote na si mali kitu! Inasikitisha sana kuona baadhi ya Media wanashabikia jambo wasilolijua na kudhani yakua ghorofa ni kitu cha maana sana kuliko sanaa yetu, utambulisho wetu na fahari yetu sasa na hata kizazi na kizazi. Nyumba ya sanaa ilikua inawapeleka wanafunzi nchi za nje kujifunza sanaa iweje leo si chochote miongoni mwetu? jengo lenyewe pekee ni sanaa tosha, je? ni Sanaa ipi mnayoitaka ionekane pale? nduguzangu tujaribu kuongea ya msingi, ya kujenga na si kubomoa kila kitu hata kama bado ni cha msingi, inashangaza!!! Nawaomba wana habari wachunguze kwanza kabla hawajaropoka ropoka hewani na kujiona wao ndio mwisho wa mambo yote, mnatutia aibu sana mbele ya jamii na hata kimataifa. Michoro iliyoizunguka nyumba ya sanaa ni ya mkongwe George Lilanga! MTAFUTENIN KWENYE GOOGLE mtaona shujaa aliye wapigania mbaki kwenye ramani ya sanaa na leo hii hamuoni sanaa yoyote katika jengo lile! Acheni siasa nduguzangu tufanye kazi iwe kazi na wala isiwe mradi kazi. Poleni sana kama imewaudhi na kwheri
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment