Thursday, October 21, 2010
Jana nimeanza safari ya kuandika Kitabu cha Babu yangu George Lilanga tarehe 20/10/2010 Natakiwa kumaliza 20/10/2011 hii tarehe ndio siku yangu ya kuzaliwa na nimeamua kusherekea siku hii kwa kazi ya kuandika kitabu ili kumuhenzi Babu yangu, na ni ahadi yangu kwake na nilazima niifanye! naomba Mungu anisaidie kwa hili, Naamini ili niwe na amani nibora nifanikishe hili ndipo nianze safari yangu ya kuandika juu ya Who is Hendrick Lilanga? Thanks a lot Marafiki wote/ Hendry Lilanga
Monday, October 18, 2010
Wednesday, October 13, 2010
Habari ndugu na marafiki pia! Kwa wale wapenzi wa kazi za mikono hususani Sanaa kwa ujumla. Napenda kuwaeleza wale wote wenye wasiwasi na kazi za G. Lilanga yakua ni feki !!! Jibu ni kwamba, hakuna picha feki za George Lilanga, kwani kazi yoyote yenye Saini ya Lilanga hiyo itakua ni picha Original. Na yeyote anae jaribu kuiga kazi za G.Lilanga na kusaini ( lilanga ) ajue anafanya kosa bila yeye mwenyewe kujua, kwani endapo angejitahidi kufanya kazi nzuri labda hata yeye angepata sifa kama za Mkongwe huyo. Natoa changamoto kwa wasanii wote wasio jiamini yakua wao ndio wao ni bora waachane na kazi za Sanaa kwani pengine wanapoteza muda bila wao kujua. So, Tinga tinga wao ni tinga tinga! wataendelea kua tinga tinga, Na Lilanga Style itabaki kua ya George Lilanga Seniour and number 2 he will be Hendrick Lilanga Juniour! Then, who will be next...( ??? ) but every one should be like that itachukua muda. Na kwaheri rafiki
Subscribe to:
Posts (Atom)